Haijakaa Sawa Lyrics – Mbosso

Haijakaa Sawa Lyrics – Mbosso: Presenting the lyrics of the song “Haijakaa Sawa” sung by Mbosso. 

Haijakaa Sawa Lyrics – Mbosso

Sasa unanuna nini?
Au unadhani hata mimi napenda
Nishazichoka na mimi
Mboga za majani kila siku mrenda

Siko juu siko chini
Niko nusu Sadoo
Si wa kumi si sabini
Ngoma ngumu bado

Kama ibada naswali sana
Usiku wa manane tena nafunga na Suna
Mambo bado bado mwana wale
Naona yanazidi kuguma

Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby

Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Chochea kuni kipenzi changu
Asubuhi tumbo likikuming’inya
Pokea kidogo changu
Tunywe chai na mkate wa ku mimina

Akili ikichoka riziki nikikosa
Najua kwako nitajiliwaza
Kama makosa nivute chumbani
Kununa nuna unajilemaza

Ustahimilivu mnao wachache mno
Jua shida rafiki wa mbivu
Baada ya dhiki mavuno
Kila jema lina maumivuu

Na kwenye waliomo tumo
Yarabi salama tupe tulivu
Penzi lisifike kikomo
Iyeee yeee eee

Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby

Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama


Haijakaa Sawa Lyrics - Mbosso

Mbosso – Haijakaa Sawa Song Details

Song: Haijakaa Sawa
Singer: Mbosso